Rapper ambaye kwa sasa ana kiki kubwa Bongo, Harmorapa
amezungumzia madai kwamba anabebwa na wimbi la kiki wala hayupo kwenye
game kudumu.
Hakijatosha, Harmorapa alipata nafasi pia kuzungumzia ishu ya
wanaomuongelea vibaya na hata kumtukana. Nilipata nafasi ya kupiga stori
na Harmo na alikuwa na la kuwaambia wanaomsema vibaya. “Watu ambao
wanahisi Harmorapa hatodumu kwenye game kwanza wanakosea halafu pia
naweza nikasema kwamba wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye
anayepanga na kupangua,” alisema rapper huyo.
Aliendelea kusema…”Kama mimi binafsi nimejipanga sana vya kutosha.
Unajua kwamba maneno yao mimi hayanivinjii chochote ni ile sawa na
kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo. Wanavyoniongea mimi ndo
wananipa power na wananipa maujuzi na wananipa kuweza. Ni wao
wananiweza mimi kuweza na kukaza ilmradi niweze kufanya kazi nzuri.”
Katika hatua nyingine nilitaka kujua iwapo Harmonize amemjua kabla
awe supa staa au vipi. Alinijibu kwa kusema kwamba hakuwa akimfahamu
muimbaji huyo kutoka WCB kabla hajakuwa staa. Wakati akiendelea kufanya
vizuri na wimbo wake wa ‘Kiboko ya Mabishoo’, Harmorapa amewaahidi
mashabiki wake makubwa mwaka huu na amewataka wawe tayari kushuhudia
maangamizi atakayofanya kwenye game mwaka huu.
HARMORAPA AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE KIMUZIKI....ADAI WANAOMTUKANA WANAMPAISHA.
Reviewed by Unknown
on
7:05 AM
Rating: 5