Msanii wa filamu Aunt Ezekiel amefunguka kwa kudai kuwa ameshawahi kutoa mimba kadhaa lakini hajui ni ngapi.
Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Cookie, akijibu
swali la shabiki wake kupitia Kikaango cha EATV aliyetaka kujua idadi ya
mimba ambazo amewahi kutoa, Aunty alisema hawezi kusema uongo kuwa
hajawahi kutoa mimba, lakini kitu ambacho hakumbuki ni idadi ya mimba
alizowahi kutoa.
“Kutoa nishawahi, nikisema sijawahi nitakuwa muongo, ila kukumbuka ni mimba ngapi ndiyo tatizo,”alisema staa huyo wa filamu.
Muigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na dansa wa
Diamond Platnumz, Mose Iyobo, amesema kwa sasa anatamani zaidi kupata
mtoto wa kiume atakamuita jina la Greyson ambalo ni jina la babu yake.
Aunt Ezekiel Akiri kuwahi Kutoa mimba...Bofya hapa kumsikia Live
Reviewed by Mipiko
on
8:37 AM
Rating: 5