PICHA: Baada ya Kutoka Rumande....TID amuweka wazi Mpenzi Wake Mpya
Msanii mkongwe wa muziki TID ameamua kusahau yaliyopita na
kuanza maisha mapya ikiwa ni siku chache toka aachiwe na mahakama kwa
sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 na kutakiwa kuripoti polisi kwa
mwezi mara mbili baada ya kukiri kutumia Madawa ya kulevya pamoja na
wenzake 12.
Muimbaji huyo ambaye alikaa lupango kwa siku tano kabla ya kuachiwa,
amemtangaza mpenzi wake mpya ambaye jina lake halikutambulika mara moja.
“The Smile i needed to see after all the trouble i have been through.
Million Dollar Smile, am i in Love again!,”aliandika TID Instagram huku
akaiwa ameweka picha ya mrembo huyo hapo juu.
Aliongeza, “Watasema sana na kisha watalala kama kunipenda najua unanipenda sana ooohyeahhh,”.


