Nuh Mziwanda Akesha Akiomba Mapacha

Msanii wa muziki Bongo, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa
anakesha kila siku akimuomba Mungu amjaalie mke wake Nawal ambaye sasa
ana mimba ya takriban miezi minne ajifungue watoto mapacha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Nuh alisema kuitwa baba wawili
imekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu na anaomba itimie kwa mkewe huyo
kipenzi. “Niseme tu wazi kwamba natamani sana mke wangu ajifungue
mapacha.
Naamini furaha yangu itakuwa zaidi ikiwa hivyo lakini hata akiwa mmoja
pia nitashukuru. Kikubwa naomba mke wangu ajifungue salama ili na sisi
tuingie kwenye ulimwengu wa wazazi,” alisema Nuh.
Nuh alifunga ndoa na Nawal mwishoni mwa mwaka jana na ilielezwa kuwa,
wakati mwanadada huyo akiolewa alikuwa tayari ameshanasa mimba.


