Baada ya mwenyekiti wa Yanga, Yusuf
Manji kuachiwa kwa dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi ya kutumia
dawa zakulevya, Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amempongeza
mwenyekiti huyo.
Kupitia akaunti yake Instagram, Wema
ameshindwa kuzizuia hisia zake baada ya kuweka picha ya Manji pamoja na
kuandika maneno machache ya kumpongeza bada ya kupata dhamana hapo jana.
Manji ambaye ni mfanyabiashara maarufu
nchini alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo aliachiwa kwa
dhamana ya shilingi milioni 10.
Wema alindika kama ifuatavyo huku
akiambatanisha na picha ya mwenyekiti huyo. “Alhamdulillah… I said it
once and I’ll say it again… What doesnt Kill you only makes you
Stronger…. On behalf of Young africans niseme tu Asante Mungu kwa
kututolea Manji wetu ndani.. Mule ndan sio sehemu nzuri kabisa jamani…
Na anaekupeleka kule hawezi kua rafiki hata kidogo… Tena wa kukaa nae
mbali kabisa… Inshallah all will be well… Nimefurahi kwakweli… Kama
kawaida sitaki maoni… And naona hii ndo iwe mfumo mpya… Turn off
comments basi… All in all, Welcome Back!”
Manji na Wema Sepetu ni miongoni mwa watu
waliotajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kuelvya ambao walitakiwa kufika
kituo cha polisi makao makuu (Central) makuu jijini Dar es Salaam.
Huu hapa Ujumbe wa Wema Sepetu baada ya Manji kuachiwa kwa dhamana Kisutu
Reviewed by Mipiko
on
5:28 PM
Rating: 5