MSANII BABY MADAHA AMPA TANO RC MAKONDA NA HARAKATI ZA DAWA ZA KULEVYA

Mwanamuziki
Baby Joseph Madaha amefungukia uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul
Makonda wa kuanza kudili na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya
akisema kuwa, huenda ikasaidia mastaa wengi kubadilika.
hivi
karibuni, Baby Madaha ambaye naye aliwahi kukwaa skendo ya kudaiwa
kusafi risha unga kwenda Uarabuni, alisema kuwa anajua kweli mastaa wengi
ni watumiaji na wasafi sharisha wa unga hivyo kitendo cha baadhi yao
kutaitiwa, kinaweza kuwa mwanzo mzuri.
“Niliwahi
kudaiwa kusafi risha unga lakini haikuwa kweli. Wanaouza na kutumia
wanajulikana, hivyo mimi nimpe tu tano Makonda kwa hatua hii nzuri,
naamini huko tuendako jitihada hizi zitazaa matunda,” alisema Madaha


