Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi amesema watamchukulia hatua muwekezaji aliyetoa
ardhi kwa serikali ya mkoa wa dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda kwa kuwa ardhi aliyoitoa siyo yake.
Lukuvi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar
es Salaam na kufafanua kuwa muwekezaji huyo aliidanganya serikali pamoja
na kumdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye ndiye
aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya serikali.
Mbali na kosa la kuidanganya serikali
Lukuvi pia amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki
ardhi kinyume cha sheria.
Kuhusu Mkuu wa Mkoa , Paul Makonda,
Lukuvi amesema tayari amekwishafanya naye mawasiliano na kumuelewesha
kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda,
huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya serikali.
Siku ya Jumanne wiki iliyopita Makonda
alikabidhiwa ekari 1500 za ardhi na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate
Mohamed Iqbal kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vigogo nchini,
katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano
hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo alisema
wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli
za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa
kati.
Kwa upande wake Makonda aalieleza kuwa
dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo,
hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji,
utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote.
Lukuvi Acharuka kuhusu Ardhi aliyopewa Paul Makonda Kisarawe II
Reviewed by Mipiko
on
5:53 PM
Rating: 5