Waziri wa maji, mazingira na
mpango wa ardhi wa Burundi Emmanuel Niyonkuru ameuawa kwa kupigwa risasi
mapema leo majira ya saa 12:45 asubuhi alipokuwa njiani kurudi nyumbani
kwake.
Msemaji wa polisi wa nchi hiyo Pierre Nkurikiye amesema
hayo kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa, waziri huyo amepigwa risasi
akiwa anarudi nyumbani kwake eneo la Rohero.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amesema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakayepatikana na hatia ya mauaji hayo.
Waziri wa mazingira wa Burundi auawa
Reviewed by Mipiko
on
3:02 AM
Rating: 5