Mchekeshaji Masele Chapombe kapata jiko

Mwishoni
mwa wiki hii ameaga ukapera baada ya kufunga ndoa na mchumba wake,
Specioza Malick iliyofungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira
Maria Consolata lililopo Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya mashabiki walitoa maoni yao kuhusu ndoa yao na kumshauri Mrembo huyo
ajitayarishe kucheka zaidi na wakati huohuo awe na ubavu wa
kutenganisha kazi ya Masele na maisha halisi.
Muigizaji Masele, amekuwa msanii wa kwanza kufunga ndoa ndani ya mwaka 2017.








