Mnajimu, Maalim Hassan Yahya Hussein ametabiri vifo vya viongozi
mbalimbali wa kidini, kisiasa, wasanii pamoja na wanahabari kama
vilivyotokea kwa mwaka 2016.
Hassan Hussen ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari jiji Dar es Salaam kuhusu utabiri wake wa mambo
mbalimbali yatakayotokea mwaka huu.
Akiwa katika mkutano huo alitaja baadhi ya mambo ambayo anaamini
yatatokea mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutokea kashfa kubwa sana ya
ngono au fumanizi itakayowahusu viongozi wa dini, siasa na wasanii
maarufu itakayosababisha viongozi hao kufedheheshwa na kuanguka kabisa
katika tasnia zao.
Alisema pia kuwa, viongozi wakubwa wa upinzani duniani na Tanzania
watarejea kwenye vyama walivyovihama miaka ya nyuma kutokana na sababu
mbalimbali. Mwaka huu pia kutakuwa na vifo vya viongozi wakubwa maarufu
wa kisiasa na kidini, baadhi ya vifo vitakuwa ni vya ghafla ambavyo
vitasababishwa na msongo wa mawazo na shinikizo la damu.
Vifo vya vya ghafla vya wasanii maarufu duniani ikiwemo Tanzania vinaweza vikatokana na fumanizi au kuuliwa au kuuana wenyewe.
Pia alisema moto mkubwa utatokea nchini na duniani.
Isikupite Hii:Mtabiri Atabiri Vifo vya Viongozi wa Dini, Siasa, Wasanii na Wanahabari Tanzania....Sababu za Vifo vyao zatajwa
Reviewed by Mipiko
on
8:24 PM
Rating: 5