USALAMA WA DAWA AINA YA “DICLOFENAC” NA “DICLOPAR”
1. TFDA inajukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kudhibiti
ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya
usalama wa dawa aina ya “Diclofenac” kupitia mitandao ya kijamii kama
ilivyojitokeza mwaka 2013.
3. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda tena kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana
kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs” (NSAIDs) ambazo
hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa
mbalimbali kama magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi namaumivu ya
kichwa.
b. Mamlaka imesajili dawa yaDiclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani
na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake na
hivyo dawa ya Diclofenacinayotumika nchini ni salama kwa matumizi ya
binadamu. Aidha, tunapenda kusisitiza kuwa dawa yenye jina la kibiashara
la Dicloparina mchanganyiko wa viambato hai vya Diclofenac na
Paracetamolimesajiliwa na TFDA na ni salama kwa matumizi ya binadamu.
c. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara
yanayofahamika ikiwa ni pamoja na kusababisha vidonda vya tumbo,
kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.
d. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, Mamlaka ya Udhibiti wa
Dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya(European Medicines Agency yenye makao
yake jijini London, Uingereza)ilitoa tahadhari kwamba watu wenye
matatizo ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata
kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa
moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo
wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda
mrefu.
4. Kufuatia taarifa hiyo, sanjari na mifumo ya ufuatiliaji wa madhara
yatokanayo na dawa nchini, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo
na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na
nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara
yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana
katika vituo vyote vya afya nchinipamoja na kutumia mfumo mpya wa
Kielektroniki unaopatikana katika simu za mkononi aina ya “Android”
kupitia anuani ya mtandao: www. tfda.go.tz/adr
5. Mamlaka inashauri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua
tahadharizamadhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo
la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara
ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.
6. Vile vile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila
kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
TAARIFA Kuhusu Usalama Wa Dawa Aina Ya “Diclofenac” Na “Diclopar
Reviewed by Mipiko
on
6:54 PM
Rating: 5