Mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kiume wa tuzo za EATV
2016, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amefunguka kwa kuweka wazi mipango yake
ya kazi ambayo itamfanya afanye mambo makubwa katika tasnia ya filamu
kama aliyofanya marehemu Steven Kanumba.
Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa katika uzinduzi wa video mpya ya
Belle 9, Gabo amedai tayari ameanza kuhudhuria workshop mbalimbali za
maswala ya filamu ili kuangalia namna ambavyo anaweza kuipeperusha
vizuri bendera ya Tanzania kimataifa.
“Ukiachana na mtazamo mdogo ambao watu wanautazama kuhusu tasnia ya
filamu, ukiingia katika website yangu utaanza kuona jinsi
ninavyojibrand, afanya bishara online, tayari kuna mawasiliano makubwa
ya watu wa nje na ndani. Lakini kutumia nafasi hiyo hiyo tayari kuna
mianya midogo midogo ambayo imenifanya nifanye workshop ndogo ndogo
ambazo nimeanza kuhudhuria ili kuangalia wenzetu wanafanya vitu gani,”
alisema Gabo.
Muigizaji huyo ambaye yupo chini ya Kampuni ya Vitamin Music Group
Limited ya msanii wa muziki Belle 9, amedai mipango hiyo ni ishara tosha
ambayo inaonyesha nini anaenda kukifanya katika miaka ijayo.
Gabo Aahidi Kurejesha Heshima ya marehemu Kanumba....Tazama Video hapa Chini
Reviewed by Mipiko
on
9:15 AM
Rating: 5