Video:MSIKILIZE MODEL CALISAH AKIFUNGUKA MAZITO KUHUSU WEMA SEPETU
Mwanamitindo
aliyejipatia jina mwaka huu kutokana na kuwa na uhusiano wa muda mfupi
na Wema Sepetu, Calisah, amemwelezea muigizaji na Miss Tanzania huyo wa
zamani kuwa ni msichana mzuri na mwenye mapenzi ya kweli.
“Wema
ni msichana mzuri, ana upendo, ni mwelewa, ana mapenzi ya kweli,
sijaona kasoro kubwa ambayo yeye anayo kubwa tofauti na wasichana
wengine,” amesema Calisah. “Ni msichana anayejua kucare, ana real love,
pia ana mapungufu yake lakini mazuri ni mengi,” amesisitiza.
Model
huyo ameongeza kuwa kwa sasa yeye na Wema hawazungumzi tena baada ya
wiki kadhaa zilizopita kusambaa mtandaoni video inayowaonesha
wakibusiana kwa mahaba mazito, kitu ambacho kilimkera Wema na kuvunja
uhusiano wao.
Hata hivyo Calisah amekiri kuwa uhusiano wake na Wema umemuongezea umaarufu zaidi na kumrahisishia kazi zake.
"Kuwa
na Wema imeniongezea kitu nisiwe muongo,” anasema. “Sababu nimekuwa
nafahamika mpaka nje ya mipaka ya Tanzania, Kenya, Uganda, kwahiyo
imenisaidia. Pia imenirahisia kwenye kazi zangu ninazofanya, hilo
namshukuru Mungu japokuwa tumeishia vibaya, umaarufu umekuja wakati
mbaya.”


