Benki Kuu ya Tanzania(BoT) yatolea ufafanuzi kutotumika tena noti ya shilingi 500
Benki
Kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa habari
inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi
mia tano haitatumika tena baada ya Disemba 31, 2016 sio taarifa ya kweli
na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki BoT, Marcian Kobello
ambapo alifafanua kuwa noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika
mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo
itakapotoweka mikononi mwa wananchi.
Aidha, Kobello amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazoeleza vinginevyo kwani si za kweli.



