Mamlaka ya viwanja vya ndege
nchini Kenya KAA ilifunga kwa muda uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta JKIA
baada ya ndege moja ya Somalia kupata ajali wakati wa kutua kwenye
uwanja huo jana usiku.
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imesema ajali hiyo imeathiri
kuruka na kutua kwa ndege kwenye uwanja huo mjini Nairobi, lakini hakuna
abiria aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.
Maofisa wa mamlaka hiyo wamesema ndege moja kutoka Somalia ilitua kwa dharura kwenye uwanja huo na kwenda nje ya barabara.