Wakazi wa Bunju Beach wahakikishiwa ulinzi na usalama.
SUALA
la wizi na ujambazi kwa wakazi wa Bunju Beach kubakia kuwa historia
baada ya Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni kuahidi kujenga kituo cha
Polisi kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua Askari zaidi ya 40.
Hayo
yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan
Kaganda alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua umoja wa Wakazi
wa Bunju “Bunju Beach Community Support” .RPC
Kaganda amesema kuwa wezi na majambazi wamekula kwao na kuongeza kuwa
suala la ulinzi na usalama ni la kila raia kwa mujibu wa sheria.
Awali
akisoma risala ya Jumuiya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya
kusaidiana ya Wakazi wa Bunju (Bunju Beach Community Support), Vanessa
Milinga alisema kuwa Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na lengo
la kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na familia za wakazi wa Bunju
Beach.
Vanessa
amesema kuwa mwaka 2011 walipata usajili ambapo pia wanachama
wameongezeka na kupelekea kubadili kuongezeka kwa malengo ambayo ni
pamoja na kuanzishwa kwa SACCOSS.
Akizungumzia
historia ya Bunju Beach Community Support, Mmoja wa waanzilishi wa
Jumuiya hiyo Profesa. Joas Rugemalila amesema kuwa umoja huo umeanzishwa
kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi, usalama, amani na maendeleo.
RPC
wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumza na wanajumuiya ya Bunju Beach
Community Support wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya
hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya
Bunju Mhe. Phocas Nato, OCD Kawe, John Malulu na Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
Makamu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach,Bunju Beach Community
Support Bi. Vanessa Milinga akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa
hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hivi karibuni Jijini Dar es
Salaam.
RPC
wa Kinondoni Suzan Kaganda akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa
Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach (Bunju Beach Community Support) Bi.
Vanessa Milinga mara baada ya kumkabidhi risala wakati wa hafla ya
kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
Muasisi
wa Jumuiya ya Bunju Community Support Profesa. Joas Rugemalila
(kushoto) akigonga cheers na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakati wa
hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar
es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
RPC
wa Kinondoni Suzan Kaganda wakigonga cheers wakati wa hafla ya
kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.


