MWIMBAJI wa muziki wa Kizazi Kipya, Najma Dattan amesema hawezi kutumia
“kiki” yoyote kwa ajili ya kupata umaarufu, akidai kwamba sura yake ni
“kiki” tosha. Najma ambaye ni mchumba wa msanii Barakah Da Prince,
alisema ameamua kuweka wazi jambo hilo kufuatia lawama ambazo zimekuwa
zikielekezwa kwake, zikiwemo za kudaiwa kutafuta “kiki” kwa kuwaharibia
wenzake.
“Mimi huwa sifanyi kazi kwa “kiki” na kwa sasa chochote
nitakachokisema naweza nisieleweke hivyo nimeamua bora nikae kimya tu,
lakini ukweli ni kwamba mimi mwenyewe ni “kiki” tosha,” alisema kimwana
huyo mwenye asili ya mchanganyiko ya Mhindi na Mbongo.
Alikuwa
akizungumzia tofauti ambazo zilijitokeza hivi karibuni kati yao na
boyfriend wake wa zamani, Mr. Blue aliyekuwa akiwatuhumu Najma na
Barakah kwamba walitaka kumharibia ndoa yake kwa kumzushia mambo ya
uongo.
MCHUMBA WA Baraka da prince ASEMA HAITAJI "KIKI" YOYOTE... adai sura yake ni "kiki" tosha
Reviewed by Mipiko
on
5:02 PM
Rating: 5