Breaking News

Ludovic Utouh ashauri taasisi mbalimbali kujiunga na soko la hisa nchini




Aliyewahi kuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania LUDOVIC UTOUH ameziomba taasisi mbalimbali kujiunga katika soko la hisa.
Uttoh ameyasema hayo Jijini Dar es salaam katika utoaji Tuzo kwa taasisi mbalimbali zilizofanya vizuri kwenye ukuaji wa hisa zao katika soko hilo Taasisi ambazo ni NMB,CRDB,MAENDELEO BANK,TBC,CITZEN na OBY SECURITY.

UTOUH amesema ni vyema sasa Taasisi  nyingine kuiga mfano huu ulionyeshwa na taasisi nyingine nchini kujiunga na soko la hisa Tanzania.

“Soko hili lilianzishwa baada ya semina waliyofanya Arusha ivyo ni soko change na makampuni yaliyopo katika soko hilo ni machache hivyo ni vyema kwa Taasisi zetu kujiunga katika soko hili ili kujenga uchumi bora kwa Taasisi nan chi kwa ujumla”ameeleza UTOUH.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utoaji wa Tuzo msajili wa hazina LAURENCE MAFURU amesema kuwa ili soko hilo la hisa liweze kukua linapaswa kutambua na kushinikiza utawala bora Zaidi na pia kuna umuhimu nwa kutoa elimu kwa taasisi mbalimbali ili kuweza kuelewa umuhimu wa soko hilo nchini.

Aidha Mkurugenzi wa soko la hisa nchini Tanzania MOREMI MARWA amesema kuwa wana mpango wa kushawishi taasisi nyingine nyingi iweze kujiunga na soko hilo la hisa ili kukuza uchumi wa Taasisi hizo na Taifa kwa ujumla ambapo amesema kuwa wanatarajia baada ya miaka 20 soko kukua Zaidi na kuweza kujitanua katika maeneo mbalimbali