Ikiwa
mgogoro wa kiuongozi unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF)
umefikishwa mahakamani kwa ajili ya kupatikana suluhu ya kisheria. Chama
hicho kimedai kusikitishwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi kwa madai
kuwa lina mlinda aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahim
Lipumba kwa kushindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria
baadhi ya wafuasi wake, iliyodai kuwa walifanya fujo katika mkutano mkuu
wa chama hicho, walivamia ofisi kuu ya chama na wale waliohusika na
jaribio la utekaji wa Naibu Katibu Mkuu wake Joran Bashange.
Chama
hicho kimedai kuwa, kiliripoti kesi zaidi ya mbili kwa jeshi la Polisi
lakini hadi sasa hakuna shauri hata moja lililofunguliwa dhidi ya
wahusika, na kudai kuwa badala yake limekamata wanachama wake 23
waliokuwa wakitokea Zanzibar kwa madai ya kuimarisha ulinzi, na
kuwapeleka mahakamani.
Naibu
Mkurugenzi wa Uenezi na Habari CUF, Mbarara Maharagande amewaambia
waandishi wa habari kuwa chama hicho kinashangazwa kwamba, hadi sasa
Polisi haijafikisha watuhumiwa hao mahakamani na wala hakuna shauri
lolote lililofunguliwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Maharagande
amedai kuwa “Kiitendo kinachofanywa na jeshi la Polisi ni cha ukiukwaji
wa sheria, sisi chama tumesikitishwa na mwenendo wa jeshi hilo sababu
linaonyesha kuna watu wanaotakiwa kushughulikiwa haraka, na wapo
wanaolindwa ili wasichukuliwe hatua za kisheria.”
Amedai
kuwa, katika tukio la jaribio la utekaji wa Bashange lililotokea
Septemba 16, 2016 watuhumiwa wake walifikishwa katika kituo cha Polisi
cha Buguruni kisha kuachiwa huru, pia amedai kuwa gari ambalo ndiyo
kielelezo cha ushahidi wa tukio hilo limeondolewa kituoni hapo.
“Gari
la ushahidi lilotumika katika siku ya jaribio la kutekwa naibu katibu
wetu, limeondolewa katika kituo cha Buguruni, watuhumiwa wako huru
inaonyesha kuna ubabaishaji katika jeshi la Polisi. Hata hivyo katika
masijala ya DPP hakuna shtaka la jaribio la utekaji wa Jorani Bashange,”
“Kesi
za mwanzo ziko wapi? Lipumba alifanya fujo Agosti 21, 2016 na wafuasi
wake tuliripoti hakuna mashtaka, baadhi ya walinzi wake walifanya
jaribio la utekaji lakini waliohusika wako huru, walivamia ofisi hakuna
shauri lililofunguliwa, walisema yako kwa DPP lakini tulipofuatilia
tulikuta hakuna mashitaka,” amesema.
Amedai
kuwa “Suala hili linahusiana na kadhia ya jinai vilivyofanywa na
wafuasi wa Lipumba,mashitaka tuliyapeleka katika vyombo vya dola yaani
jeshi la polisi na mpaka sasa watuhumiwa wa makosa hayo hawajafikishwa
katika mahakama, badala yake walipeleka mahakamani wanachama wetu 23
ambao ni walinzi waliotokea zenji kuja kushirikiana na wa bara kulinda
ulinzi wa chama. Tumestaajabishwa kwa nini tuhuma za nyuma
hazijashuhulikiwa.”
Maharagande
ameeleza kuwa, siku ya Jumatatu baadhi ya viongozi wa CUF walikwenda
katika ofisi ya ZCO ili kujua maendeleo ya mashauri yaliyofunguliwa na
chama hicho, na kwamba walielekezwa kwenda katika ofisi ya DPP kwa kuwa
ndipo mashauri hayo yalipofunguliwa.
“Tuliambiwa
hakuna shauri linalohusiana na watu wa nne waliohusika na jaribio la
utekaji wa naibu katibu mkuu wetu, itambulike kuwa, maelezo ya kuja kwa
DPP tumeyapata katika ofisi ya ZCO kwa hiyo Jumatatu tulilazimika kwenda
kujua limefikia wapi shauri hilo ndipo tulipofika tukaambiwa hakuna
kinachoendelea,” amesema.
Hata
hivyo, Joran Bashange amesema waliitwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa
lakini walikakataa kujieleza, na kudai kuwa walibaini kwamba wanataka
kupewa tuhuma mpya.
“Walitaka
kutuhoji kwa tuhuma tusizozifahamu, na ndio wito tulioitiwa lengo la
wito lilikuwa kutufungulia mashtaka mapya ambayo hatujayafahamu,
walituambia kwamba wamepokea malalamiko kutoka kwa Lipumba, sisi
hatukutaka kuwajibu zaidi ya kuwaambia kesi ya Lipumba iko mahakamani
kisheria hatuwezi ongea au kutoa maelezo yoyote kuhusu Lipumba,”
amesema.
Licha
ya tuhuma hizo, Bashange amedai kuwa wamepata taarifa ya kwamba
kutokana na ukata wa fedha, wafuasi wa Lipumba wameanza kuuza mali za
ofisi ya chama zilizopo Buguruni Jijini Dar es Salaam.
“Sasa
hivi Lipumba hana fedha za kulipa wafanyakazi, kuna ukata na
wameshaanza kuuza mali za ofisi ili wapate fedha za kujikimu,” amesema
Bashange ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi CUF.
CUF yalia na Polisi kuhusu Lipumba, yadai wafuasi wake kuuza mali za chama
Reviewed by Mipiko
on
7:25 PM
Rating: 5