Waziri Nape Nnauye kutua ndani ya TFF

Akiwa TFF kuanzia saa 4:30 asubuhi, Waziri Nape atazungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF imewaalika katika ziara hiyo.
Katika ratiba hiyo, Nape ataoneshwa maendeleo ya michezo hususani mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya Airtel na kuratibiwa na TFF ambako kwa mikoa mbalimbali iliyofanya vema, kesho timu za wanawake na wanaume zitacheza hatua ya nusu fainali kabla ya fainali za Jumapili ambazo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


