Breaking News

Vita ya Panzi Furaha ya Kunguru Nchini Sudan Kusini


Waandishi wa ripoti hiyo yenye kichwa, Udhaifu wa Vita Haustahili Kujilipa, walisema kuwa walichunguza uhusiano uliopo kati ya wakuu nchini Sudan Kusini na pesa zilizonunua nyumba za kifahari na biashara nyingi za madini, mafuta na za kifedha.

Shirika la Sentry linawalaumu Rais Salva Kiir, kiongozi wa upinzani Riek Machar na majenerali wakuu jeshini pamoja na familia zao kwa kunufaika wakati mamilioni ya watu nchini humo wamekuwa wakitaabika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tofauti za wanasiasa waku wawili zilisababisha kutokea mapigano yaliyozuka mwezi Disemba mwaka 2013.

Ripoti moja ilisema kuwa , inaonekana watu wachache wanadhibiti asilimia kubwa ya uchumi wa Sudan Kusini na wengi wa watu hawa ni wale walio madarakani.