Ripoti ya kamati ya
bunge nchini Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa
kuingilia kati na kusaidia kuondolewa mamlakani kwa Kanali Muammar
Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.
Kamati hiyo ya Mambo ya Nje
imesema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo
zingewakumba raia baada ya serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na
maasi.
Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumiwa kama fursa ya kubadilisha utawala, ripoti hiyo inasema.
Inamtuhumu aliyekuwa waziri mkuu David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahsusi kuhusu Libya.
Wabunge
hao wanasema hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa
wenyewe, mzozo wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kukua
kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika
kaskazini.
Msemaji wa serikali ya Uingereza ametetea serikali
na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, pamoja na Umoja
wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.
Gaddafi aliuawa na waasi 20 Oktoba, 2011.
Ufaransa na Uingereza zalaumiwa kwa kuangusha utawala wa Gaddafi Libya
Reviewed by Mipiko
on
9:11 AM
Rating: 5