Serikali ya Somalia imeondoa marufuku iliyokuwa imewekwa dhidi ya mirungi kutoka nchi jirani ya Kenya.
Mirungu ambayo pia hufahamika kama miraa, hutumiwa sana Somalia lakini huwa haikuzwi huko.
Uamuzi
wa kuondoa marufuku hiyo iliyowekwa wiki iliyopita ulitangazwa baada ya
marais wa nchi hizo mbili, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Hassan Sheikh
Mohamoud, pambizoni mwa mkutano wa IGAD.
Mkutano huo wa muungano
wa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na pembe ya Afrika ulikuwa wa
kwanza kuandaliwa mjini Mogadishu tangu kuanzishwa kwa muungano huo.
Usafirishaji
wa mirungi hadi Mogadishu, biashara ya thamani ya karibu dola nusu
milioni kila siku, inatarajiwa kurejelewa Jumatano.
Marufuku
iliyokuwa imewekwa iliwaumiza sana raia wanaoitumia pamoja na
wafanyabiashara nchini Somalia sawa na wakuzaji nchini Kenya.
Bei ya mirungi ilikuwa imepanda pakubwa.
Ndege
15 za kusafirisha miraa huingia Mogadishu kila siku zikiwa zimebeba
magunia 12,000 ya miraa ya thamani ya $400,000 (£298,000) kwa mujibu wa
mtetezi wa haki za wauzaji miraa Somalia Abukar Awale.
Somalia yahalalisha Mirungi kutoka nchini Kenya
Reviewed by Mipiko
on
9:24 AM
Rating: 5