Breaking News

Tanzania kuzindua mpango wa kitaifa wa kutafiti HIV

Tanzania kuzindua mpango wa kitaifa wa kutafiti HIV




Serikali ya Tanzania imesema ina mipango ya kuzindua utafiti wa nchi nzima kuhusu viashiria vya HIV / UKIMWI na athari zake ili kubaini kiwango cha maambukizi mapya nchini humo
Mwanatakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Emilian Kerugendo, amesema utafiti huo, utazinduliwa Septemba 14 mjini Dodoma, na kuendelea kwa kipindi cha miezi minane.
Alisema utafiti huo utakuwa tofauti na zile za nyuma za mwaka 2003/2004, 2007/2008 na mwaka 2011/2012 kwani hasa utajikita kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49.
Kerugendo alisema utafiti utafanywa katika maeneo 525 yaliyotambuliwa nchini kote, ukishirikisha watu 16,000, na watoto angalau 8,000.
Alisema walengwa watapimwa VVU / UKIMWI, hepatitis, kaswende, kiwango cha CD4, na usugu wa dawa.