Breaking News

Marekani yaadhimisha miaka 15 tangu shambulizi la 9/11 litokee


Marekani imeadhimisha miaka 15 tangu shambulizi la kigaidi la 9/11 kwa njia tofauti kwenye sehemu mbalimbali nchini humo.

Akitoa hotuba kwenye bustani ya kumbukumbu ya tukio hilo iliyoko wizara ya ulinzi, rais Barack Obama amesema tishio la ugaidi linaloikabili Marekani kwa sasa limebadilika, kwa kuwa magaidi wanajaribu kupanga mashambulizi madogo lakini yenye athari kubwa. Rais Obama amesisitiza kuwa, watu wa tamaduni tofauti kuishi kwa pamoja ni chanzo cha nguvu cha Marekani, na kuwataka wananchi washikamane na kutoruhusu vitendo vyovyote vya kuleta mfarakano nchini humo.

Baadhi ya jamaa wa wahanga wa tukio hilo wameeleza kutoridhika na sera ya sasa ya serikali katika kupambana na Ugaidi, wakiona nchi yao iko hatarini zaidi kuliko wakati lilipotokea shambulizi la 9/11.