Hudson Kamoga wa Clouds Tv ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya
Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.
Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-
- Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
- Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
- Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
- Bakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
- Juma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
- Butamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
- Waziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
- Fatma Omar Latu – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
- Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma
- Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
- Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
- Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe


