Breaking News

Mourinho ashika nafasi ya Pili duniani kwa makocha wanao lipwa Mkwanja mrefu zaidi, Zidane, Klopp hawaoni ndani

Jose Mourinho amekuwa kocha wa pili duniani katika mchezo wa soka kulipwa fedha nyingi zaidi baada ya kuanguka saini ndani ya klabu ya Tottenham ambayo itakuwa inampatia kiasi cha pauni milioni 15 kwa mwaka.
Kusaini kwake tu, kwa miamba hiyo ya soka ya Kaskazini mwa jiji la London, Mourinho atakuwa anapokea kitita cha fedha mara mbili ya mshahara ambao alikuwa akilipwa kocha aliyetimuliwa kazi, Mauricio Pochettino.
Hii ni kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya Tottenham, kumwajiri kocha mwenye kariba ya Mourinho ambaye tayari ameshinda mataji 25 kwenye taaluma hiyo huku wakitoa kitita kinono.
He still trails Pep Guardiola though with the Manchester City boss on a £20m-a-season deal
Mourinho sasa atakuwa akipokea mshara wa Pauni Milioni 15 kwa mwaka kiasi ambacho kinamfanya kushika nafasi ya pili (2), kwa malipo ambayo wanapa makocha wanaofundisha mchezo wa soka.
Mreno huyo anakuwa nyuma ya Pep Guardiola ambaye anashika nafasi ya kwanza akipokea Pauni Milioni 20 baada ya kuongeza mkataba wake ndani ya Manchester City msimu uliyopita 2018 ambao atashuhudiwa akiwa hapo kwa miaka mingine miwili.
Mhispania huyo ndiyo kinara kwa makocha wote wa soka duniani akipokea kiasi hicho cha pesa pauni milioni 20 kwa mwaka na akidhihirisha uhalali wa yeye kupokea mkwanja huo baada ya kuchukua ubingwa wa Premier League ‘back-to-back’.

TOP 10 HIGHEST-PAID MANAGERS

1. Pep Guardiola – Manchester City (£20m)
2. Jose Mourinho – Tottenham (£15m)
3. Diego Simeone – Atletico Madrid (£13m)
4. Rafa Benitez – Dalian Yifang (£11.5m)
5. Fabio Cannavaro – Guangzhou Evergrande (£10m)
5. Zinedine Zidane – Real Madrid (£10m)
7. Antonio Conte – Inter Milan (£9m)
8. Thomas Tuchel – PSG (£8m)
8. Ernesto Valverde – Barcelona (£8m)
10. Jurgen Klopp – Liverpool (£7m)