”Kamwe siwezi kuifundisha Tottenham, nawapenda sana mashabiki wa Chelsea”-Kauli ya Mourinho 2015, je ni nini kimembadili ?
Jose Mourinho amekuwa kocha mpya wa Tottenham licha ya kuwa mwaka 2015 aliwahi kusikika akisema kuwa kamwe hatakuwa mwalimu wa timu hiyo kutokana na heshima yake kwa Chelsea.
Mreno huyo ambaye amewahi kuifundisha Chelsea na kuipatia mataji mawili hatimaye amechaguliwa kuwa kocha mpya wa wapinzani hao wa London hapo jana siku ya Jumanne kufuatia kufukuzwa kazi kwa Mauricio Pochettino.
Wakati wa fainali ya ‘League Cup’, mwaka 2015 Chelsea ikiikabili Tottenham kwenye dimba la Wembley, Mourinho amesema amekuwa akihitajiwa Mwanyekiti wa Spurs, Daniel Levy ili kuyabeba majukumu ya White Hart Lane mwezi Septemba 2007.
Na ndipo, Mourinho amesema 2015 kwamba kamwe hatokuwa kocha wa Tottenham, hii ni kutokana na hisia zake kwa Chelsea.
Lakini pia ameafikiana na Chelsea kwamba hatokuja kufundisha klabu nyingine za Uingereza kwa miaka miwili ijayo baada ya kuja kuachana na The Blues.
Alipoulizwa kuwa aliwahi kuhitajiwa na Spurs mwaka 2007, Mourinho alisema ni kweli ”Ni kweli, lakini sikuenda, wala sikuwa na klabu nyingine hapa Uingereza kwa muda wa miaka miwili. Sikuchukua kazi yoyote kwa sababu ya kuwapenda mashabiki wa Chelsea.” Mourinho ameipatia Chelsea mataji matatu ya Premier League, FA Cup na matatu ya League Cups.