Kundi la muziki la Navy Kenzo lapishana kauli na msanii wa WCB Harmonize
Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili ambao wapo kwenye mahusiano ambao ni Aika na Nahrel wiki iliyopita ya septemba 27 walifanikiwa kuachia wimbo wao mpya unaojulikana kwa jina la “Katika” ambao wamemshirikisha C.E.O wa WCB Wasafi Diamond Platnumz.
Licha ya kuwa kimya kwa mda kidogo baada ya Aika kupata ujauzito na kufanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume sasa wamerudi rasmi kwenye muziki baada ya kutoa ngoma hiyo inayoendelea kufanya vizuri kwa sasa huku wakiahidi kuachia ngoma zingine kali sana.
Baada ya wasanii hao kuachia nyimbo yao hiyo ya Katika inayoendelea kufanya vizuri kwa sasa,ziliweza kutokea tetesi za kuwa wasanii hao kusainiwa na lebo hiyo kubwa ya muziki ikiwa chini ya Diamond ya WCB.lakini baada ya wasanii hao kuulizwa swali walipinga vikali huku wakisema wao wako chini ya meneja Sallam ambaye pia ni meneja wa Diamond na sio Wasafi,tetesi hizo zilianzia pale ambapo msanii mwingine wa WCB Harmonize kuandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa “Navy Kenzo karibuni Usafini” na kudai kuwa yeye hapendi vitu vya siri kwani hawamuogopi mtu yeyote lakini baada ya Harmonize kumaliza maneno hayo Nahrel alijibu na kuonyesha kuiunga mkono kauli hiyo ya Harmonize.