Mzee Majuto ampa mtihani Rais Magufuli na Waziri Mwakyembe
Mchekeshaji Mkongwe nchini Tanzania, Mzee Majuto amefunguka kuwa kwa sasa hana lengo la kuendelea na sanaa hiyo tena.
Mzee Majuto amedai kuwa maamuzi hayo ni ya mwisho na hakuna mtu yeyote atakayemsikiliza kwa sasa isipokuwa Rais Magufuli na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Majuto amesema haoni sababu ya kuendeleea kuigiza lakini anategemea ushauri kutoka kwa viongozi hao wakubwa nchini Tanzania kama watamwambia aendelee kuigiza atafanya hivyo ila hakuna mtu yeyote zaidi ya hao atakayemshauri kuhusu hatma ya sanaa yake.
“Natoa kauli kwamba nastaafu na hii kazi, labda Rais wangu Mpendwa Rais John Pombe Magufuli au Mzee Mwakyembe waniambie hapana endelea ndio nitaamua kuendelea,“amesema Mzee Majuto kwenye kipindi cha eNEWS cha EATV na kueleza sababu zake.
“Hakuna mtu mwingine wa kunishauri, baba yangu ameshafariki, mama yangu ameshafariki na marafiki zangu wote ni Wasanii watupu.“amesema Mzee Majuto.

Mwaka jana Mzee Majuto alitangaza kustaafu kazi hiyo na kuahidi kuwa ataendelea kufanya matangazo tu kwa makampuni yatakayomuhitaji.