Mfahamu kikongwe wa miaka 80 ambaye ni fundi wa radio za magari
Mfahamu kikongwe wa miaka 80 ambaye ni fundi wa radio za magari
Bibi huyo maarufu kwa jina la ‘Shosh’ ameonekana kuwa tofauti na watu wenye umri kama wake ambao maranyingi huishi majumbani na kuwategemea watoto wao au hata wajukuu kuwalisha lakini kwa Cecilia ni tofauti kabisa.
Kwa mujibu wa BBC bibi Cecilia anaduka lake la kuuza, kurekebisha na kuweka upya radio za magari lililo barabara ya Outering mjini Nairobi, huku akiwa mwenye shughuli nyingi kwa wateja kuhitaji huduma yake.
Akizungumza na chombo hicho cha habari bibi Cecilia amesema kuwa amekuwa ni mtu wa kujishukhulisha kwa shukhuli mbalimbali tangu miaka ya 70.
Mimi nilizaliwa Nairobi na nimefanya biashara kadhaa tangu miaka ya sabini na hata nilikuwa na gari langu.Nilikuwa nimeajiri dereva na kondakta lakini mara nyingi walikuwa wananilaghai wakinidanganya kuwa gari limeharibika ninawapa pesa lakini hawanunui vipuri. Ndipo nikaamua nifanye kazi ambayo nitakuwa naisimamia mimi mwenyewe
Cecilia anaonekana bayana kuwa na ujuzi wa juu kuhusu mambo ya radio za magari kulingana na jinsi anavyoelezea na kushughulikia wateja wake.
Anasema licha ya yeye kutokuwa na kisomo chochote alianza kujifunza taratibu kuanzia mwaka 1991 kukarabati na kufunga radio za magari kwa fundi mmoja mara nyingi kwa kuangalia tu jinsi kazi hiyo ilikuwa ikifanywa.
Fundi aliyenifundisha aliniambia ninunue vifaa vichache tu ambavyo nilitumia kujifunzia hii kazi na tangu wakati huo nimeifanya kazi hii kwa miaka yote hii, ni kazi ninayoifurahia kwa saabu ninaipendaKila wakati ninahakikisha kuwa wateja wangu wameridhika na huduma yangu na pia ninawazungumzia kwa njia nzuri ndio wapate kurudi tenaKazi ni kazi, hakuna kazi ya kufanywa na mwanaume au mwanamke, hata kama ni ya kupaka viatu rangi rangi, ni kazi inayoweza kufanywa na kila mtu, kwa hivyo mtu asichaguae kazi
Bibi Shosh ana vijana kadhaa wanaomsaidia na kazi kwenye duka lake na baadhi yao ni wajukuu wake ambao anasema anataka awasaidie kujimudu kimaisha na waweze kujitegemea siku za usoni. Wateja wengi wanaofika duka la Shosh hutaka huduma yake mwenyewe.
Anasema siri kuu ambayo imechangia yeye kuwa kwenye biashara hii kwa kipindi kirefu kama hiki na wateja kumpenda ni kuwa mkweli kwa kazi yake na kuwaheshimu wateja.
Anasema biashara hii imemwezesha kujikimu kimaisha. Anawashauri watu wote, wanaume kwa wanawake, wasichana kwa wavulana wasichague kazi.
Pia anasema kuwa kufanya kazi kwa uaminifu imekuwa nguzo muhimu kwa biashara kwa kazi yake. Ni lazima kila wakati ahakikishe kuwa ana leseni zote zinazohitajika kwa biashara yake ili kazi yake iweze kuendelea. Licha ya umri wa miaka 80 Cecilia anasema ana ndoto kubwa ya siku za usoni.
Ni lazima nihakikishe kuwa duka langu lina leseni na hata bango lililo nje ya duka na ni lazima nililipie ili kuhakisha kuwa ninafanya biashara bila ya usumbufu wowoteNingependa siku moja niwe na shule ya kuwafunza vijana kazi hii ya ufundi wa redio. Niwe na shule ambayo mimi mwenyewe nitahakikisha kuwa nimempa mwanafunzi cheti baada ya kuhitimu vizuri
Bibi Cecilia ameongeza kuwa kamwe hana mpango wa kuachana na kazi hiyo siku za hivi karibuni hatakama Mungu atambariki kuishi miaka 200.