Breaking News

IGP Sirro afanya mabadiliko Makamanda wa Polisi

Ikiwa imepita siku moja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kumuapisha Waziri wa Mambo ya Ndani mteule, Kangi Lugola. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi kwa baadhi ya Mikoa.

Taarifa iliyitolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, imesema mabadiliko haya yanalenga kuongeza juhudi za kuzuia ajali zilizotokea mara kwa mara katika baadhi ya Mikoa.
Mabadiliko ya Makamanda wa Jeshi la Polisi.
1. SACP Deusdedit Nsimeki aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anakwenda kuwa RPC Simiyu.
2. SACP Ulrich Matei aliyekuwa RPC Morogoro, anakwenda kuwa RPC Mbeya.
3. Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya, ACP Mussa Taibu amehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
4. SACP Wilbroad Mutafungwa aliyekuwa RPC Tabora, anakwenda kuwa RPC mkoa wa Morogoro.
5. ACP Emmanuel Nley kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, anakwenda kuwa RPC Tabora.
6. ACP Stanley Kulyamo aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Geita anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.
Soma taarifa kamili: