Wabongo kuwa nao makini sana, ndio wanapenda kiki – Weusi (+video)-Hassbaby Blog
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Nikki wa Pili amesema idadi kuwa ya mashabiki wa muziki/Wabongo ndio wanapenda kiki na ndio sababu ya wasanii kuendeleza dhana hiyo
Video source>: Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi ambalo kwa sasa linatamba na ngoma ‘Mdundiko’, amesema kama wasingekuwa wanapenda basi kusingekuwa na kiki.
“Watanzania watakuambia hawapendi kiki lakini ndio habari za kwanza kuzifuatilia. Na watu ambao wanafanya hayo mambo ndio wenye followers wengi, kwa hiyo kuwa makini na wabongo sana” amesema.
“Watakuambia hawa wasanii watu wa kiki lakini ndio watu maarufu na wanao-trend kila mahali, kwa hiyo wanaojidai kuwashambulia wasanii tuache,” Nikki wa Pili ameiambia Bongo5.
Nikki ameendelea kwa kusema Kiki ni namna msanii anavyotaka ku-push product (muziki) yake sasa itategemea hiyo kiki ni ya namna gani. Kiki ambayo itakuwa ya ubunifu, itatumia akili na sanaa hana tatizo nayo.
Kwa upande wake Joh Makini amesema; ‘Inategemea na kiki unayofanya, chochote unachofanya siunajua ni jinsi gani kitakulipa, kwa hiyo ni kufikiria mara mbili mbili aina ya kiki inaweza kuwa na madhara kiasi gani kwa upande wako,’.