Breaking News

Mali ya Yahya Jammeh kuuzwa kupitia mtandao

Serikali ya Gambia inapanga kuuza ndege za kifahari pamoja na magarai ya rais wa zamani Yahya Jammeh kwa njia ya mtandao.
Nchi majirani waliingilia kati kumtimua madarakani Rais Jammeh baada ya kushindwa kwenye uchaguzi Disemba mwaka 2016 ambapo alikataa kuondoka madarakani.
Aliacha nyuma ndege tano na magari 30 ya kifahari, yakiwemo ya Rolls-Royce na Bentley pamoja na mashamba manne, kwa mujibu wa AFP.
Mwaka uliopita serikali ilisema kuwa ina nia ya kupata mamilioni ya dola kutokana na kuuzwa kwa mali ya Jammeh na kuwekeza fedha hizo katika sekta za afya na elimu.
"Kile tunafanya kama serilali ni kuwa na tovuti ambapo mali hayo yote yatachapshwa," Lamin Camara, katibu katika wizara ya fedha aliiambia AFP.
Tarehe ya kuuzwa kwa mali hiyo bado haijatangazwa.
Yahya Jammeh