Mayweather kuinunua Newcastle na kumsajili Ronaldo
Mwanamasumbwi mwenye sifa, mikogo na majivuno makubwa nchini Marekani, Floyd Mayweather amekuja na jipya wiki hii baada ya kudai anaweza kuinunua klabu ya Newcastle United ambayo ipo sokoni kwa sasa na kumshawishi mchezaji bora wa dunia na mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo kumalizia soka lake lakulipwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Mwanamasumbwi raia wa Marekani, Floyd Mayweather
Mayweather ambaye ni bondia machachari awapo ndani na nje ya ulingo na anayetamba zaidi kuwa na fedha za kutosha amesema kuwa anafikiria kufanya uwekezaji katika soka.
Klabu ya Newcastle imekuwa kwenye harakati za kupata mmiliki mpya baada ya Mike Ashley kusemekana kuvunja mazungumzo kati yake na Amanda Staveley ya kuinunua timu hiyo.

Ni vyema ukaamini kuwa ningeweza kuwekeza, ningekuwa na kwenda mara kwa mara bondia huyo amekieleza chombo cha habari cha the Star siku ya Jumapili.
Nimekutana na baadhi ya wachezaji wa Newcastle mwaka jana, niwatu wema. Siku zote naanzisha nafasi za biashara na napenda michezo yote lakini nawekeza kutokana na kichwa changu kinavyonituma na siyo kutoka moyoni.
Kuwekeza kutoka ndani ya moyo ni rahisi kupata hasara lakini mtu akijitokeza na kushirikiana katika mipango ya kibiashara ni rahisi kutengeneza fedha, hivyo ningependa kuwekeza katika soka hatakama siyo mchezo wangu kwakuwa nina watu kila sehemu.