WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ATOA AGIZO KALI KWA WAKAZI WA MKOA WA KAGERA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka watumishi wa Umma na wananchi wa wilaya ya Misenyi waishio karibu na mpaka wa Mutukula kutoshirikiana na wahalifu kukamilisha mambo yao kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa na hatua kali zitachukuliwa juu yao hasa wanaohusika na kuwaingiza wahamiaji haramu.
Hayo ameyasema akiwa ziarani mkoa wa Kagera wilaya ya Misenyi katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Mutukula) kukagua utendaji kazi wa idara ambazo zipo chini ya wizara yake na changamoto zinazozikabili kwa ajili ya kuzitatua ili kumaliza kabisa tatizo la wahamiaji haramu nchini.
Waziri Mwigulu amewaahidi idara ya uhamiaji na polisi kuwaletea magari ambayo yatasaidia katika kufanya ukaguzi katika maeneo ya mpakani na pia atawaletea rasilimali watu kuongeza ufanyaji kazi zaidi.
Naye mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis Filangali Mwila amesema kwasasa wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa vitendea kazi kwa idara ambazo zipo mpakani ambapo inachangia kuingizwa kwa bidhaa kwa magendo na kupitisha wahamiaji haramu ambao wanatoka nchi za jirani.