Breaking News

  

KWA HIKI ALICHOKIANDIKA DIAMOND KUHUSU ZARI BASI HAKUNA KUACHANA TENA

Wengi walidhani Diamomd Platinumz na Zarina Hassan wameachana kabisa. Lakini hii imebaki kama ndoto baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja katika mitaa ya maraha. Katika kutilia mkazo zaidi Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram ameamua kuwazima wabaya kwa kuwahakikishia kuwa Zari ndiye mtunza siri wake na kuahidi kutomuacha milele.

"Wee hodari mtunza siri zangu hata nikiwa sina, hunivumilia na kuamini nitapata....nakuapia hakiamungu sitokuacha" aliandika Diamomd

Naye Zari the boss lady baada ya kuona ujumbe huo alijibu mapigo kwa kumshukuru Diamond kutokana na jinsi alivyosifiwa na tayari dunia nzima imezimwa fikra kwamba wawili hawa wameachana.