TANZANIA YA VIWANDA YAMUIBUA GAVANA WA BoT....ASHAURI MAMBO MANNE YA KUZINGATIWA
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ametaja maeneo manne yanayopaswa kuzingatiwa kwa Tanzania kukua kiuchumi na kufikia ndoto yake ya kuwa ya kipato cha kati.
Ameainisha maeneo hayo muhimu katika kitabu chake alichokiandika kwa kushirikiana na mchumi mwandamizi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Nkunde Mwase kinachoitwa: “Tanzania: The Path to Prosperity” ambacho kilizinduliwa hivi karibuni.
Katika kitabu hicho, Profesa Ndulu anapendekeza kutumika kikamilifu kwa rasilimali zilizopo ili kuamsha kasi ya uendelezaji viwanda na sekta nyingine za uzalishaji na kuweka mkazo kwenye kilimo kinachowagusa wananchi wengi.
Pia, anataka kuchukuliwa hatua thabiti za kuimarisha sekta ya huduma na kuwekeza kwenye miundombinu na rasilimali watu.
Hoja za Profesa Ndulu zinakuja wakati Serikali ikiwa katika kampeni ya kukuza viwanda ili kuimarisha uchumi na kufikia malengo ya kuwa taifa la kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Tanzania ipo katika mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP2) ulioanza mwaka 2016/17 mpaka 2020/21.
Kilimo
Ndani ya kitabu hicho, hoja kubwa inayojadiliwa ni uwekezaji zaidi kwenye kilimo ambayo ni hatua muhimu inayoweza kuleta matokeo chanya ya kuondokana na umaskini.
“Sera zinazohusu kilimo na usindikaji zinapaswa kutiliwa mkazo katika kuboresha uzalishaji, kuimarisha mtaji hasa usafirishaji na kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija kwa kukabiliana na mabadiliko yoyote yakiwamo ya tabianchi na kuwa na soko la uhakika,” anasema Profesa Ndulu.
Profesa huyo aliyeiongoza BoT tangu mwaka 2008, anasema mkazo uwekwe katika kukaribisha mbinu mpya za kilimo na kuwekeza kwenye utafiti ili kuwa na kilimo cha kisasa chenye uzalishaji wa manufaa.
Ripoti ya mwenendo wa uchumi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonyesha kuwa kati ya Januari hadi Machi, ukuaji wa sekta hii ulishuka kutoka wastani wa asilimia 2.7 mpaka asilimia 2.6 ndani ya mwaka mmoja.
Maliasili
Kwa kutambua nchi nyingi zenye utajiri wa asili zilivyotumbukia kwenye laana hivyo kujikuta zikiwa na demokrasia haba na, mafanikio duni kiuchumi na kijamii tofauti na nchi zenye rasilimali chache, wasomi hao wanaamini Tanzania ina fursa nzuri ya kutumia vyema rasilimali zake kujinufaisha.
Hata hivyo, kupata mafanikio hayo wanasema itahitaji kuwa na mkakati mahsusi ambao utajieleza vyema namna itakavyozitumia. “Gharama za biashara zinapaswa kuwa shindani na mazingira ya kufanya biashara yawe rafiki. Ukiritimba kwenye usajili na maeneo ya ufanyaji biashara uondolewe,” kinaeleza kitabu hicho.
Serikali imefanya mabadiliko muhimu ya kisera na sheria kuhakikisha wananchi na taifa wananufaika zaidi. Kwenye Bunge la Bajeti lililomalizika, sheria tatu zilifanyiwa mabadiliko kufanikisha hili.
Katika utekelezaji wake, mazungumzo kati ya Serikali na kampuni ya Acacia inayoongoza kwa uchimbaji wa dhahabu yanaendelea kwa takribani miezi miwili sasa.
Sekta ya huduma
Profesa Ndulu anabainisha kwamba, kuboresha sekta ya huduma kutaiwezesha Serikali kufikia ndoto yake ya kukuza uchumi. Wanataka kuwepo mkakati wa kuongeza uelewa wa utoaji taarifa katika baadhi ya huduma kama ya utalii. Anaunga mkono dhana iliyopo kwa muda mrefu kutoka kwa wadau wengine kwamba sekta ya utalii ni eneo ambalo bado halijaendelezwa kwa kiwango kinachotakiwa ili kuongeza mchango kwenye Pato la Taifa (GDP).
Takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonyesha kuwa watalii walioingia nchini mwaka jana waliongezeka kwa asilimia 12.9 kutoka zaidi ya watalii milioni 1.137 mwaka 2015 hadi zaidi ya milioni 1.284.
Haya yote yametokea licha ya Serikali kuanzisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyoanza kutozwa Julai, 2016. Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa na jitihada za kutangaza vivutio vilivyopo kwa soko la kimataifa na msisitizo ukielekezwa kwenye utalii wa ndani pia.
Hivi karibuni, bodi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) ilizindua video ya vivutio inayoonyeshwa kwa abiria wa mikoa ya Kusini.
Sekta hiyo imeajiri wastani wa watu 500,000 moja kwa moja huku zaidi ya milioni moja wakiwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Miundombinu
Kitabu hicho kinasema Serikali inatakiwa kubuni sera itakayoongeza msukumo wa kuwekeza zaidi katika miundombinu ili kupata matokeo chanya kiuchumi. Kinapendekeza Serikali ibuni vyanzo vingine kugharimia uwekezaji huo.
Wanapendekeza vyanzo vya ndani vichanganywe na vya nje kufanikisha ajenda hiyo.
Serikali imekuwa ikifanya hili kwa muda katika jitihada za kuimarisha miundombinu ya usafiri na uchukuzi. Kwa kutumia vyanzo vya ndani, imeanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro huku ikitafuta wabia watakaofanikisha kuikamilisha mpaka Kigoma na Mwanza.
Profesa Ndulu na Mwase wanasema Tanzania inapaswa kuwa na ‘mkakati jumuishi’ utakaoimarisha miundombinu ya mawasiliano kuanzia reli, anga, barabara na bandari.
Licha ya miradi mingi inayotekelezwa maeneo mbalimbali nchini, ripoti ya robo mwaka ya NBS inaonyesha ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa asilimia 8.4 kati ya Januari na Machi ikilinganishwa na asilimia 8.6 za kipindi kama hicho mwaka jana.
#Mwananchi