Breaking News

RAIS MAGUFULI AELEZA MASIKITIKO YAKE BAADA YA TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea namna ambavyo ameshtushwa na taarifa za kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu ambaye ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Rais Magufuli ameandika ujumbe wenye masikitiko makubwa huku akivitaka vyombo vya dola kuwasaka wale wote waliohusika na unyama huo na kufikishwa katika mikono ya sheria.

"Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha katika mikono ya sheria" aliandika Rais Magufuli.