PICHA:TUNDU LISSU APIGWA RISASI...TAZAMA HAPA BAADHI YA PICHA KUTOKA ENEO LA TUKIO
Taarifa kutoka Dodoma zinaeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa TLS Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana leo hii. Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari muda mfupi uliopita zimedai kuwa tukio hilo la kusikitisha limetokea eneo la Area "D" mkoani Dodoma.
Baadhi ya picha za gari la Mhe. Tundu Lissu zikionesha matundu ya risasi
Taarifa hiyo ilieleza kwamba Mhe. Tundu Lissu anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea kuimarika kutokana na kwamba kuna timu ya madaktari katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambao mpaka sasa wanahangaika na hali ya mbunge huyo.
Naye mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Dodoma alipoulizwa swali na mwandishi kwamba ni maeneo gani mbunge huyo amejeruhiwa kwa risasi alijibu kwamba kuna timu ya madaktari bingwa ambao mpaka hivi sasa wanaendelea kupambana na afyaya Mhe. Tundu Lissu na baadaye watakuja na taarifa kamili ambayo itaeleza kwa kina kuhusu tukio hilo ikiwa ni pamoja na sehemu mbalimbali zilizojeruhiwa za mbunge huyo.
"Kuna timu ya madaktari bingwa ambao wanaendelea kumfanyia matibabu na baadaye watakuja na taarifa kamili ambayo itaeleza sehemu za mwili wa Mhe. Tundu Lissu zilizojeruhiwa kwa risasi...."alisema mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya picha za gari la Mhe. Tundu Lissu zikionesha matundu ya risasi