Breaking News

PICHA:AITELEKEZA FAMILIA YAKE NA KUFUNGA NDOA YA KIFAHARI NA NG'OMBE

Hapa duniani ukisikia usemi huu "ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni!" basi firauni kapatikana. Baba mmoja mfugaji nchini India amewatelekeza mkewe na binti zake wawili kwa kudai kuwa hana furaha kuishi nao kwenye nyumba moja na kuamua kufunga ndoa ya kifahari na Ng’ombe.
Baba huyo aliyetambulika kwa jina la Vijay Parsana (44) amechukua uamuzi huo baada ya kukosa faraja kutoka kwa mkewe akidai kunyanyaswa na familia yake.

Parsana amesema hata alivyokuwa yupo kwenye ndoa na familia yake alikuwa akikaa na ng’ombe muda mwingi akifanya nao mazoez, pamoja na kuwaogesha kila siku huku akitumia mkojo wa ng’ombe kama chai kila asubuhi na jioni.

Baba huyo  aliyeitelekeza familia yake katika kijiji cha  Ahmedabad, na kukimbilia katika tarafa ya Sarawat mjini Gujarat nchini India, amedai kwa sasa ameisahau kabisa familia yake na maisha yake yote anaamini kuwa alizaliwa kuishi na wanyama.

Mapema mwezi julai mwaka huu Bwana Parsana aliwashangaza watu nchini India alipochukua uamuzi wa kufunga ndoa na ndama wawili wakike, kwa kutumia dola $20,000 ambapo kwenye harusi hiyo alialika marafiki na ndugu wapatao elfu tano.
“Ng’ombe wangu nawapenda sana upendo wangu kwao hauelezeki hakuna nimpendae zaidi ya wanyama wangu, huwa nikiwa nao kitandani nasahau shida na mateso yote duniani, tayari tumetengeneza uhusiano mzuri na naona kama wanafamilia wangu wapya na hata mke wangu amekubali niendelee kuishi hivi baada ya kugundua naishi kwa amani kuliko nilivyokuwa nae, kwani wamekubali na wanatambua upendo wangu kwa wanyama ndio maana tukatengana“,amesema Bwana Vijay Parsana kwenye mahojiano yake na gazeti la Ahmedabad Mirror.

Bwana Parsana kwa sasa anamiliki Ng’ombe 50, mbwa sita, Sungura 15, Tausi 8 na nyoka 3 na hutumia dola $5,000 kila mwaka kwenye sherehe ya wanyama wake pindi wanapotimiza miaka ya kuzaliwa.
“Hawa ng’ombe nawaheshimu sana kama mama yangu, utajiri wote huu nilionao nimeupata kutoka kwa hawa ng’ombe sioni taabu kuwatengenezea sehemu nzuri ya kulala,“amesema Parsana.

Mkewe na Bwana Parsana, Bi. Geeta Parsana wakati wapo kwenye mahusiano alifikiri mmewe amepatwa na kichaa baada ya kuongeza upendo na ng’ombe wake kiasi kwamba huenda nao hadi kwenye mazoezi.

“Nilianza kumuona kama chizi alipoanza kutembea na ng’ombe hadi kwenye mazoezi kipindi tukiwa wote alikuwa mnyonge sana akikosa kuwaona ng’ombe wake tulipotengana baada ya miaka miwili alionekana mwenye afya tele na mafanikio makubwa kiuchumi basi haikuwa bahati kuwa naye nasisi kama familia tunafurahi kumuona akiwa na afya,“amesema Bi. Geeta Parsana.

Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya India kuhusu maamuzi hayo ingawaje sheria nchini humo zinaruhusu watu kuishi na wanyama pori kama Tembo nk.Tazama baadhi ya picha za matukio mbalimbali ya maisha ya Bwana Parsana (Photo Credit- CAP)
 
Bwana Parsana akiwa kwenye gari na ng’ombe wake siku ya sherehe za harusi .