Breaking News

MBUNGE WA MOSHI VIJIJINI AIOMBA SERIKALI KUONGEZA BAJETI KWENYE SEKTA YA ELIMU

Wanafunzi wa shule ya msingi assumpta iliyopo KIA wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro wamejumuika kufanya sherehe ya kuhitimu mafunzo yao ya elimu ya msingi iliyofanyika shuleni hapo mapema Jumamosi ikiwa ni hatua yao ya kwanza katika maisha yao ya shule.

Akizungumza wa wageni waalikwa pamoja na wahitimu hao mgeni rasmi mheshimiwa Anthony Komu ameiomba jamii kubadilisha mtazamo hususani katika suala la elimu ili kuleta maendeleo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Komu ameongeza kuwa jamii inatakiwa kubadilika kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma mpaka vyuo vikuu lakini ajira zinakuwa hazipo hivyo amewataka wazazi kuwa wazalendo kwa kuwapeleka watoto kwenye vyuo vya ufundi kusomea fani mbalimbali kulingana na vipawa vyao.

Hata hivyo ameomba serikali kutenga bajeti kubwa katika sekta ya elimu ili kuhakikisha huduma za elimu zinaboreshwa na  zinawafikia wanafunzi kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka elimu ya juu ili kushindana na mataifa mbalimbali  ulimwenguni hususani katika suala la utandawazi

Pia mkuu wa shule hiyo Bi.Yohana  Furia ameeleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo katika suala la uendeshaji wa shule hiyo ikiwa ni pamoja na ushirikiano mdogo  wa wazazi katika kulipa ada kwa wakati jambo ambalo linapelekea baadhi ya huduma kutopatikana kwa wakati na kile kidogo kinachopatikana kinaelekezwa kwenye huduma za muhimu kama chakula,maji na umeme.

Wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi shuleni hapo kwa mwaka 2017  ni 30 ambapo wavulana wakiwa 16 na wasichana 14 ambapo shule inafanya vizuri kwa mitihani ya taifa ya darasa la nne na la saba.
Mtazame hapa chini👇👇👇akifunguka zaidi.