WANANCHI WA MKOA WA KILIMANJARO WAOMBWA KUCHANGAMKIA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI
Meneja wa mfuko wa bima ya Afya wa Taifa Bw.Fidelis Shauritanga |
Meneja wa mfuko wa bima ya afya wa Taifa( NHIF )mkoa wa Kilimanjaro bw. Fidelis Shauritanga amewaomba wananchi wa mkoa huo kujiunga na huduma mbalimbali za mfuko wa bima hiyo ili kuboresha afya zao.
Akizungumza
na Efm ofisini kwake mapema hivi leo amesema kuwa wananchi wa mkoa huo wamekuwa
wakinufaika na huduma za mfuko wa bima ya afya wa taifa kupitia vituo vya
serikali,taasisi na mashirika ya dini pamoja na vituo binafsi.
Amesema
mpaka sasa mkoa wa Kilimanjaro vituo vilivyosajiliwa jumla yake ni 292,ambapo
vituo vya serikali ni 192,mashirika na Taasisi za dini vikiwa ni 72 na vituo vya watu binafsi ni 24.
Hata hivyo
amewahamasisha wananchi wa mkoa huo kujiunga na huduma ya toto afya kadi ambapo
huduma hiyo inamuwezesha mtoto wa umri
chini ya miaka 18 kutibiwa nchi nzima kwa zaidi ya vituo vya afya 7000 ambavyo
vimesajiliwa na mfuko huo kwa gharama ya shilingi 50400 kwa mwaka mzima.
Pia alieleza
baadhi ya changamoto ambazo anakumbana nazo katika kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora kutoka katika mfuko huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya vituo
vya afya kukosa vifaa tiba,madawa na miundombinu mibovu,
Sambamba na
changamoto hizo amesema kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa wakichelewesha michango
ya wanachama jambo ambalo hupelekewa baadhi yao kukosa huduma kwa wakati pindi
wanapohitaji msaada wa haraka.
Alieleza kuwa
mfuko wa bima wa taifa unatoa huduma ya mikopo kwa riba nafuu hivyo ameziomba
halmashauri za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wamiliki wa vituo vya afya kuweza
kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo ili kuboresha huduma katika vituo ambapo
mikopo inayotolewa ni pamoja na madawa,vifaa tiba pamoja na mkopo kwa ajili ya
kuboresha miundombinu ikiwemo majengo.
Amezitaja
baadhi ya taasisi na mashirika ambayo yameweza kunufaika na mikopo hiyo ikiwa
ni pamoja na KCMC Moshi,kituo cha afya Mawenzi pamoja na Same hospital.