Breaking News

SERIKALI YA CHINA YAMPONGEZA UHURU KENYATTA KWA KUCHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA KENYA

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema China inampongeza Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Kenya, na inapenda kushirikiana na Kenya kuhimiza uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya.
Bibi Hua Chunying amesema, China na Kenya ni nchi marafiki, wenzi na ndugu wazuri.