Breaking News

  

MABUNGE YA CHINA NA UGANDA YAKUBALIANA KUSHIRIKIANA ILI KUIMARISHA SEKTA MBALI MBALI

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang jana katika eneo la Beijing alikutana na spika wa bunge la Uganda Bi.Rebecca Kadaga, na kukubaliana kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya mabunge ya nchi hizo mbili. 

Bw. Zhang amesema bunge la umma la China na Bunge la Uganda yanapaswa kushirikiana kuweka mazingira bora ya kisheria kwa ajili ya biashara kati ya nchi hizo mbili. Kwa upande wake, Bi. Kadaga amesema bunge la Uganda liko tayari kushirikiana na bunge la umma la China kukuza ushirikiano kwenye sekta za kilimo, elimu na uhifadhi wa mazingira.