BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bwa. Bernard Hezron Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bima ya Taifa ya Afya (NHIF).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Bernad Hezron Konga umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Bernad Hezron Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Agosti, 2017