Breaking News

  

BREAKING NEWS: POLISI DAR WAUA JAMBAZI MMOJA, WENGINE WATIWA MBARONI

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limemkamata mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi katika msako ambao umefanyika hivi karibuni maeneo ya Vijibweni.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo Agosti 11, 2017, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar, Lucas Mkondya amesema kuwa jambazi huyo alikamatwa akiwa nyumbani kwake.

“Tulimkamata mmoja ambaye alitupeleka mpaka nyumbani kwa huyo mwenzake, alipotuona tupo na jamaa yake akaingia ndani akarudi na bastola. Lakini kabla hajatushambulia maaskari walimuwahi wakampiga risasi ya bega, tukampokonya silaha. Alianza kuvuja damu nyini tukampeleka Hospitali ya Vijibweni lakini bahati mbaya alifariki,” alisema Kamanda Mkondya.

Aidha kamanda Mkondya ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata magunia ya bangi, kete zinazodhaniwa kuwa ni za dawa za kulevya pamoja na mtandao wa wezi wa magari jijini humo ambapo watuhumiwa wote bado wanaendelea kuhojiwa na mara tu upelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.