UNICEF YASEMA WAFANYAKAZI WAKE WATATU WASHIKILIWA NCHINI SUDAN KUSINI
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema wafanyakazi wake watatu wanashikiliwa na mamlaka za kijeshi huko Pagak, makao makuu ya kundi la waasi la SPLA-IO linaloongozwa na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar.
Msemaji wa UNICEF amesema wafanyakazi watatu wa shirika la Montrose lililopewa kandarasi na UNICEF kufanya uchunguzi wa elimu kwenye eneo la Mathhing, walishikiliwa mara baada ya kufika wilaya ya Pagak Julai 6.
UNICEF imetoa wito kwa kundi la SPLA-IO kuwaachia huru wafanyakazi hao wanaojitahidi kuboresha maisha ya watoto nchini humo.