RAIS MAGUFULI AMTEUA MTUMISHI WA UDSM KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TRA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Julai, 2017 amemteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Prof. Florens D.A.M Luoga anachukua nafasi ya Bw. Bernard Mchomvu ambaye Bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.
Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma)
Uteuzi wa Prof. Florens D.A.M Luoga unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita
11 Julai, 2017