BREAKING NEWS:UBIA WA STARTIMES NA TBC WAUNDIWA KAMATI YA UCHUNGUZI
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda Kamati ya kuchunguza ubia wa Kampuni ya Startimes na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufuatia hoja mbalimbali zilizojitokeza.
Kamati hiyo iliyoundwa na Waziri Mwakyembe itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi.
Kamati hiyo itakuwa na jumla ya Wajumbe 10 watakaochunguza utendaji wa Kampuni ya ubia ya StarTimes, ambapo watano (5) ni wa upande wa Tanzania na wengine watano (5) ni wa kutoka Star Media China.
Wajumbe wanaounda Kamati hiyo kwa upande wa Tanzania ni kama wafuatao;-
- Dkt. Hassan Abbasi (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo)
- Kyando Evod (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo)
- Frederick Ntobi (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA)
- Eng. James Kisaka (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA)
- Mbwilo Kitujime (Shirika la Utangazaji la Taifa-TBC)
Kamati hiyo imepewa hadidu za rejea takribani nane na inatakiwa kufanya kazi kwa muda wa siku saba ili kukamilisha kazi hiyo.
Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
15 Julai, 2017.